map | search | help | download | contact us | français | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Ziwa Tanganyika Ziwa Tanganyika (Ramani) lina umri mkubwa sana isivyo kawaida. Mabonde yanayolizunguka yamekuwa na maji kwa walau miaka milioni kumi na baadhi ya masimbi yaani, yaani miamba na udongo utokanao na kulundikana na kugandamana kwa udongo na takataka, yana umri wa karibu miaka milioni ishirini. Likiwa na eneo la kilometa za mraba 33,000 na wastani wa kina cha karibu meta 600, Ziwa hili pia ni kubwa sana. Ziwa lina kina cha karibu kilomita moja na nusu kwenye sehemu yenye kina kirefu zaidi na jumla ya ujazo wake wa maji ni takribani kilometa za ujazo 19,000 - karibu sehemu moja ya sita ya maji yote ya baridi duniani. Kwa wachunguzi wa mabadiliko na mageuko (ya polepole), ziwa hili ni maabara asilia ya kipekee kwa sababu viumbehai vingi vinavyoishi katika Ziwa Tanganyika havipatikani kokote kwingineko. Kuna takribani spishi (yaani aina) 300 za samaki (spishi nyingine zinaendelea kugunduliwa). Theluthi mbili kati ya hizo zinapatikana kwenye ziwa hili tu. Familia yenye mafanikio makubwa zaidi, ni ile ya Cichlidae. Familia hiyo ina spishi zaidi ya mia mbili na zote isipokuwa tano hupatikana katika Ziwa Tanganyika tu. Pamoja na kiwavi mashuhuri wa maji ya baridi, zipo pia spishi nyingi za moluska na krasteshia na spishi mbili za nyoka wa majini zinazopatikana kwenye ziwa hili tu. Wakati idadi ya baadhi ya spishi za samaki zipatikanazo ziwani kwa kawaida ni ndogo, idadi ya samaki wa spishi sita zilizomo kwenye maji ya kina kirefu ni kubwa. Samaki hawa ni chanzo muhimu cha chakula na mapato kwa wakazi wa eneo hili. Pamoja na kuwepo kwake kwa muda mrefu, ziwa hili pamoja na viumbe vyake vyote vimo mashakani. Hali yake ya baadaye haina uhakika. Flora (yaani jumla ya mimea) na fauna (yaani jumla ya wanyama) ya ziwa huenda ikashindwa kubadilika kulingana na mabadiliko yanayosababishwa na shughuli zinazofanywa na wanadamu. Matokeo ya mageuko ya mamilioni ya miaka yanaweza yakapotea katika kipindi kifupi tu. Mradi wa Bioanuwai wa Ziwa Tanganyika unalenga kusaidia kuzuia jambo la aina hii kutokea.
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|| Home || |
| ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Authors | Feedback |