|
|
|
Usuli
Lengo la Mradi wa Bioanuwai wa Ziwa Tanganyika ni kuzisaidia nchi zinazozunguka Ziwa Tanganyika kuanzisha mfumo thabiti na unaoweza kujiendeleza wa kusimamia na kuhifadhi bioanuwai ya Ziwa Tanganyika sasa na hapo baadaye. Mradi huu ambao una makao yake makuu mjini Kigoma, kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa, ni wa miaka mitano na unatekelezwa asasi mbalimbali kutoka Burundi, D. R. Congo, Tanzania na Zambia, huku zikishauriwa na mashirika ya kimataifa. Kwa kuzishirikisha jumuiya za mahali panapoendeshwa mradi katika maandalizi ya mradi wenyewe, mkakati utafungamanisha malengo yote mawili ya maendeleo na hifadhi na unalenga kulinda maisha ya watu wa mahali hapo katika siku zijazo.
|